Katika tukio hilo leo Alhamisi asubuhi, madiwani wawili na baadhi ya wananchi wamekamatwa na polisi.
Kabla ya kutumia mabomu, polisi walitoa onyo wakiwataka wananchi na madiwani hao kutawanyika kwa amani lakini waligoma.
Madiwani
wa halmashauri mbili za Wilaya ya Geita jana Jumatano walitanga
mgogoro na GGM wakishinikiza kulipwa Dola 12 milioni za Marekani
zinazotokana na ushuru wa huduma kuanzia mwaka 2004 hadi 2013.
Walitangaza kuzuia magari ya mgodi kwa kufunga barabara na pia kufunga maji yanayoingia mgodini kutoka Ziwa Victoria.
GGM iliwatangazia wafanyakazi wake jana kutofika kazini leo kutokana na mgogoro huo.
Polisi
hivi sasa wameimarisha ulinzi kwenye maeneo ya Nungwe uliko mradi wa
kusambaza maji mgodini, eneo la uwanja wa ndege na geti la kuingia
mgodini.
Mkuu
wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi na mbunge wa Geita Vijijini, Joseph
Musukuma wameingia mgodini baada ya madiwani na wananchi kutawanywa
No comments:
Post a Comment