Mkuu wa
wilaya ya Bunda mwl. Lydia Bhupilipili amekemea tabia ya uwanzishwaji wa masoko
kiholela pasipo mpangilio kwani hali hiyo inapelekea kukosesha mapato ndani halmashauri
na serikali kiujumla.
Bhupilipili
ameyasema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisini
kwake ambapo amekemea tabia hiyo na kuwataka wataalamu wa mipango miji
kuhakikisha wanafanya kazi yao ipasavyo.
Aidha
Bhupilipili amemtaka mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa bunda Janeth Mayanja
kuhakikisha ana wasimamia wahusika wote wa mipango miji ili waweze boresha na
kusitisha uwanzishwaji wa masoko kila sehemu bila utaratibu hali inayopelekea
uchafudhi wa mazingira katika maeneo hayo.
Katika hatua
nyingine Bhupilipili amesema kuwa kwa sasa stendi mpya ya Mabasi kumekuwa na
mbanano wa magari na kushauri kwamba utengenezwe utaratibu wa baadhi ya magari
mfano yanayo kwenda nyamuswa yawe yanatokea Manjebe ili kupunguza msongamano
uliopo kwa sasa katika stedi hiyo.
No comments:
Post a Comment