Vijana katika Halmashauri ya Mji
wa Bunda Mkoani Mara wameombwa kutambua kuwa wao ni nguvu kazi ya taifa siku
zote, hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa bidii bila kubagua kazi, ili kuweza kuleta
maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla.
Ushauri huo umetolewa baadhi ya
vijana wa mtaa wa wa bank wakati wakizungumza na redio mazingira hii leo
Juma Hamis na Debora Joram wamesema vijana wasipojituma kufanya kazi kwa
bidii kauli ya kusema vijana ni nguvu
kazi ya taifa itabaki midomoni mwa watu bila vitendo vyovyote, hivyo ni wakati
wakujituma ili kauli hiyo iwe kwa vitendo.
Katika hatua nyingine vijana hao
wameiomba halmashauri ya mji wa Bunda, kuwajali vijana katika upande wa
asilimia iliyotengwa na serikali ili kuweza kusaidia katika majukumu yao ya
kujituma.
No comments:
Post a Comment