Tabia ya
baadhi ya wanafunzi wa kike wa shule mbali mbali za msingi na sekondari
wilayani bunda,mkoani mara,ya kuzunguka mitaani na kuwaomba wananchi
wawachangie fedha kwa ajili ya
kufanikisha mahafali yao kumaliza elimu ya msingi na sekondari, imekuwa kero
kwa baadhi ya wazazi na kuwaomba walimu wakuu wa shule hizo kukomesha tabia
hiyo.
Hayo yamesemwa
na baadhi ya wazazi walipozungumza na redio mazingira fm, na kuwaomba walimu
wakuu wa shule hizo kuwaita wazazi wa wanafunzi wanaohitimu katika shule hizo
ili kutafuta njia nzuri ya kufanikisha
mahafali hayo ili kuwaepusha watoto wa kike kukumbwa na vitendo vya ubakaji
kutoka kwa watu wenye nia mbaya.
Baadhi ya
wanafunzi wa kike ambao wamezungumza na na redio mazingira fm,wamekiri kupata
majaribu mengi toka kwa baadhi ya watu wanaowafikia kwa ajili ya kuwaomba
kuwachangia fedha kwa ajili ya mahafali yao,badala yake watu hao huwashawishi
kufanya nao mapenzi na kuwaahidi kuwapatia fedha nyingi endapo watawakubalia
tendo hilo.
Wakati
serikali ikipambana vikali na kukemea baadhi ya watu wanaowarubuni wanafunzi wa
kike nakuwapatia mimba,baadhi ya watu wanaoendekeza tamaa zao za mwili bado
wanaendelea na tabia hiyo na kujikuta wana waharibia masomo na kukatiza ndoto
za maisha yao ya baadae.
No comments:
Post a Comment