wazazi na walezi watakiwa kuendelea kulea vizuri watoto wao waliohitimu dara la saba mwaka huu - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Thursday, 14 September 2017

wazazi na walezi watakiwa kuendelea kulea vizuri watoto wao waliohitimu dara la saba mwaka huu

Baada ya wanafunzi wa darasa la saba kumaliza mtihani wa kumaliza elimu ya msingi nchini  mnamo septemba 7  mwaka huu, wazazi na walezi wa watoto hao wametakiwa kuendelea na ushirikiano ule ule wa kuwalea watoto hao katika maadili mema.

Hayo yamesemwa na  baadhi ya wakazi wa kata ya kabarimu  halmashauri ya mji wa bunda kwa nyakati tofauti ambapo wamesema kuwa wapo baadhi ya wazazi hujisahau kuwapa malezi mazuri watoto hao na kuwaacha wakifanya mambo yasiyo yakimaadili kama kujihusisha na vitendo vya ngono.

Mmoja wa wakazi hao bwana Thomas Ezekil amesema kuwa wazazi wanapaswa kutambua kwamba watoto hao bado ni wanafunzi na wanasubiri matokeo yao ili waendelee na masoma yao.

“sisi wazazi tunapaswa kutambua kwamba watoto hao ni bado ni wetu “

No comments:

Post a Comment