Bodi ya Filamu Tanzania imepokea
kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Muigizaji nguli Shamila Mfikirwa.
Katika Salamu zake
kwa Rais ya Shirikisho la Filamu Tanzania Bw. Simon Mwakifamba, Mwenyekiti wa
chama cha Waigizaji Ndugu Elia Mjata na wanafamilia wa filamu na uigizaji kwa
ujumla Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi.Joyce Fissoo amesema
amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba huo.
“Kwa niaba ya Bodi nachukua fursa
hii kutoa pole nyingi sana kwa familia ya marehemu kutokana na kuondokewa na
mpendwa wao, pia Bodi imeguswa na msiba huo na inawaombea wanafamilia kwa Mungu
kuwa na moyo wa subra katika kipindi hiki kigumu” alisema Bi.Fissoo.
Mwigizaji Shamila
Mfikirwa maarufu kama ‘Shamila’ amefariki dunia katika Hospitali ya Occean Road
Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Oktoba, 2017 alipokuwa akipatiwa matibabu.
Innalilah Wainna Ilayhi Rajiun.
Imetolewa na
Bodi ya Filamu Tanzania.
No comments:
Post a Comment