Zikiwa zimesalia wiki moja wanafunzi wa kidato cha
nne nchini kote kuanza mtihani wao wa taifa wazazi na walezi wametakiwa kuwa na
desturi ya kuwalea watoto wao katika maadili mema na kuacha kuwatuma kwenda
kununua mahitaji mbalimbali dukani nyakati za usiku kwani kufanya hivyo ni
kutoa mwanya kwa watoto hao kukutana na watu wanaoweza kukatisha ndoto zao kwa
kuwapatia mimba.
Hayo yamesemwa jana na mgeni rasmi katika mahafari
ya 24 katika shule ya sekondari bunda mheshimiwa diwani wa kata ya kabarimu Pastory
Ncheye.
Amesema suala la mimba linatokana na wazazi
kutowajengea malezi mazuri watoto wao, na kutolea mfano kuwa mzazi anapomtuma
mtoto kwenda kufanya biashara usiku au kununua bidhaa usiku dukani inapelekea
watoto hao kukutana na watu wanaowashawisha kushiriki nao kufanya ngono hatimae
kupata mimba.
Aidha amewatahadharisha wanafunzi kuacha kujihusisha
na vitendo vya ngono kwani kupata mimba ni majaliwa lakini watambue kwamba kuna
gonjwa hatari la ukimwi.
Mheshimiwa ncheye katika mahafari hayo ameaidi kushirikiana
na shule hiyo kurekebisha gari la shule lililoaribika kwa muda mrefu hivyo kuitaji fedha zaidi ya
shilingi milioni moja kukamilika.
Pamoja na hayo pia ncheye ameaidi kuwapelekea miche
ya miti ili kuhakikisha mazingira ya shule hiyo yanaendelea kuwa mazuri na ya kupendeza,
na kuwasifu kwa jitihada walizozifanya za usafi wa mazingira.
Kwa upande wake mwalim mkuu wa shule hiyo Machota Kora
katika risala yake amesema kuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya
upungufu wa matundu ya vyoo, vyumba vya madarasa, pamoja na uzio katika mabweni
ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita.
Hata hivyo amewaomba wazazi na walezi kushirikiana
na walimu katika kuwalea watoto kwakuwa wao wenyewe hawawezi na ndiyo maana
katika shule hiyo jumla ya wanafunzi watatu waliotakiwa kuhitimu na wanzao
walikatisha masomo yao kwa kupata mimba.
No comments:
Post a Comment