Jeshi la polisi wilayani
Bunda Mkoani Mara limewahakikishia wananchi kuwa watasherekea sikukuu kwa amani
na utulivu kwani wamejipanga kikamilrifu kukabiliana na wahalifu watakao taka
kuchafua hali ya hewa katika musimu huu wa sikukuu.
Akizungumza kupitia
kipindi cha Asubuhi leo kinachorushwa na kituo hiki Mkuu wa polisi Bunda
kamanda Jeremiah Shila amesema wao kazi yao ni kuhakikisha wanalinda raia na
mali zake hivyo katika musimu huu wa sikukuu wako makini sana katika suala la
ulinzi kaika maeneo yote ya Wilaya ya Bunda lengo ni wananchi kuwa salama
wakati wote.
OCD Shila amewatumia
salama waharifu wote wanaopanga kuja kufanya uhalifu katika wilaya ya Bunda
kuwa hata wasipoteze muda maana wao wamejiandaa kikamilifu.
OCD Shila pia amezungumzia
suala la ulinzi na usalama Wilaya ya Bunda kufuati matukio mbalimbali kutokea
hivi karibuni ikiwemo ya ukatili wa kijinsia yaliyojitokeza katika maeneo
tofauti ndani ya wilaya ya Bunda na kusema kuwa wanayafanyia kazi matukio yote
yaliojitokeza na kuomba wananchi kutochoka pindi polisi wanapotaka ushirikiano
kutoka kwao.
No comments:
Post a Comment