Mahakama ya wilaya ya Bunda MkoaniMara , Desemba
27 2017 imemuhukumu kifungo cha miaka 30
jela Baraka saimon 24 mkazi wa kijiji cha Muranda kata ya Namuhura kwa kosa la
kubaka na kumpa mimba mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16 .
Akisoma shtaka mbele ya hakimu mkaazi wa mahakama ya
wilaya ya bunda Jacklin J. Rugemalira , mwendesha mashtaka upande wa jamhuri
inspecta Masoud ameeleza mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo mnamo
tarehe 19.oktoba.2017 saa za jioni.
Aidha amesema kuwa majira hayo mtuhumiwa alimbaka
msachana huyo mwenye miaka 16 anaesoma katika shule moja ya sekondari.
Hata hivyo alipoulizwa kuhusu makosa hayo mshtakiwa
amekiri kutenda kosa hilo na ndipo mheshimiwa hakimu amemhukumu kifungo hicho
cha miaka 30 jela.
No comments:
Post a Comment