Wakazi wa
kitongoji cha Mumwaro kijiji cha Sarama A wilaya ya Bunda Mkoani Mara wameiomba serikali kuwapelekea mabwana
afya katika kitongoji hicho ili waweze kuondokana na uchafunzi wa mazingira kwa
kujisaidia ovyo aja kubwa na ndogo katika vichaka.
Kauli hiyo
imetolewa na wananchi wa kitongoji hicho walipokuwa wakizungumza na mazingira
fm.
Wambura
kigunya ambaye ni miongoni mwa wakazi wa kitongoji hicho amesema kuwa wakazi wa
kitongoji hicho walio wengi hawana vyoo kitendo kinacho wapelekea kujisaidia
vichakani bila kujua ni hatari kwa afya ya zao.
Amesema kuwa
ni vizuri kama serikali ya kitongoji ita kuwa na utaratibu wa kupita kila mji
na kukagua kama kunachoo ili kuweza kunusuru afya za wakazi wa kitongoji hicho
pia kuepuka magojwa ya mlipuko kama vile kipindupindu na kuhara.
Hata hivyo wameomba uongozi wa kitongoji hicho
kuwachukulia hatua za kisheria wale wote
watakao bainika hawana choo katika miji yao ili iwe fundisho kwa wengine.
No comments:
Post a Comment