Mama mmoja majina
tunayahifadhi anaeishi katika Kata ya Nyamakokoto halmashauri ya mji wa Bunda
Mkoani Mara ameripotiwa kumfanyia mwanae wa kumzaa kitendo cha unyanyasaji wa
kijinsi kwa kumficha ndani huku akiwa mgonjwa hali iliyompelekea mtoto huo jina
tumeliifadhi kudhoofika.
Mtoto huyo mwenye miaka 9,inaelezwa kuwa ana kg.16 tu.
Aidha afisa ustawi wa jamii
halmashauri ya mji wa bunda Pius Masalu amekiri kupata taarifa za mtoto huyo na
kuongeza kuwa baada ya kufuatilia ilibainika kuwa jina aliloandikishwa kupata
dawa hospitalini hapo ilibadilishwa mfano alikuwa anaitwa musa baadae mama yake
aliamua kubadilisha jina lake na kumwita adam.
No comments:
Post a Comment