Mkurugenzi
wa halmashauri ya mji wa Bunda Janeth Mayanja amewataka wanawake kujitokeza kwa
wingi katika uzinduzi wa saccos ya wanawake itakayozinduliwa mnamo january 4
2018 katika viwanja vya halmashauri hiyo.
Akizungumza
na redio mazingira fm, Mayanja amesema kuwa siku hiyo ya uzinduzi wataanza kwa
maandamano yakayoanzi benki ya NMB mpaka
viwanja vya halmashauri ya mji wa bunda.
Aidha
amesema halmashauri kwa kugundua kilio na uhitaji wa wanawake katika mji wa
bunda waliamua kuunda saccos hiyo itakayowasaidia wanawake kuinuka kiuchumi.
Hata
hivyo amewataka wanaume kuwaunga mkono wanawake ili kufanikisha uchumi wa
pamoja.
No comments:
Post a Comment