Baraza la
madiwani halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara limetoa siku tano kuanzia
leo kwa aliyekuwa afisa kilimo ambaye kwa sasa amestaafu kuhakikisha anatoa taarifa ya
kujitosheleza kuhusu uchakachuaji uliofanyika katika pesa ya mahindi ya msaada
yalioyogawika ndani ya halmashauri.
Azimio hilo
limetolewa leo katika kikao cha dharura cha kujadili hoja ya mkaguzi wa ndani
kutoka mkoani ambapo hoja hiyo emepelekea hadi kuimbua mambo mengine yaliyokuwa yamejificha
ndani.
Akizungumza
wakati wa kufunga kikao hicho Mwenyekiti wa halmashauri Isack Mahela amesema
wao kama wawakilishi wa wananchi hawawezi kukaa kimya wakati pesa za wananchi
zinatumika sivyo.
Hata hivyo
inaelezwa kuwa anayetuhumiwa kuhusuiana na suala hilo la pesa ya mahindi ya
msaada kupotea juu juu afisa huyo ameshasitaafu
hivi karibuni.
Awali madiwani
wameonekana kutolizishwa na majibu ya wakuu wa idara katika mambo ya msingi
yanayohusu halmashauri jambo ambalo wamesema kwa hali hiyo wataisababishia
halmashauri hati mbaya.
No comments:
Post a Comment