Siku chache
baada ya mkuu wa wilaya ya Bunda Mwl.Lydia Bupilipili kumuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa
Bunda Janeth Mayanja kuhakikisha ana wasimamia wahusika wote wa mipango miji
ili waweze kuboresha na kusitisha uwanzishwaji wa masoko kila sehemu bila
utaratibu,wananchi wa mji wa bunda wampogeza mkuu wa wilaya kwa hatua hiyo huku
wakisema ofisi ya mipango miji imejisahau katika utekelezaji wa majuku yao.
Wakizungumza
na mazingira fm kwa nyakati tofauti
baadhi ya wananchi hao wamesema kuwa wamefikia hatua ya kuanzisha masoko
kiholela pasipo mpangilio kwa sababu hawaoni watu wakuwaelekeza juu ya
upangiliaji wa mji hivyo kupelekea kukosesha mapato ndani halmashauri na
serikali kiujumla kwa sababu ya watu wachache.
Hata hivyo
wananchi hao wamesema kuwa pindi wataalam hao wataanza kuchukua hatua juu ya
suala hilo wasiyafute masoko hao bali watoe utaatibu ili kama kuanza kutoa
ushuru watu wapo tayari kufanya hivyo lakini siyo kuyafuta kabisa.
No comments:
Post a Comment