Wazazi na
walezi katika halmashauri ya mji wa Bunda Mkoa wa Mara,wameaswa kuwafundisha
vijana wao kazi za mikono za kujiajiri ili waweze kujikimu pindi wakati ukifika
wa kujitengemea wasipate shida.
Hayo
yamesemwa na Bwile Chisumu mkazi wa kata ya kabarimu mjini hapa wakati
akizungumza na radio Mazingira fm ambaye
anajishughurisha na useremala na kueleza kuwa endapo wazazi wakianza
kuwafundisha vijana wao kazi za ufundi itawasaidia pindi wakijitegemea na kuacha
kutegemea kusubili ajira kutoka serikalini.
Chisumu
ameongeza kuwa imefika wakati sasa kwa kila mwananchi kutambua kuwa kufanya
kazi ni muhimu kwa kila mtu na
kutochagua wala kuidharau kazi kwa misingi fulangi kwani kazi nzuri ni yeyote
inayokupatia kipato halali.
No comments:
Post a Comment