Zao la pamba limesisitizwa sana na serikali kuhakikisha katika
mikoa inayolima zao hilo linaongeza uzalishaji kwa kiwango kikubwa.
Katika Wilaya ya Bunda Mkoani Mara kupitia Mkuu wake wa Wilaya
mwl. Lydia Bupilipili aliagiza kila mwananchi alime hekar mbili huku akiagiza
shule zote msingi na sekondari kuwa na shamba la pamba, mbali na hivyo aliagiza
Halmashauri zote Wilaya na Mji ziwe na shamba darasa .
Katika kutaka kujuwa zaidi hatua
zilizofikiwa kupitia agizo la Mkuu wa Wilaya tumemtafuta Mkaguzi na Mratibu wa
zao la Pamba wilaya ya bunda bwana liberatus soka amesema kuwa
‘Hatua iliyofikiwa ni nzuri kwa
sababu asilimia kubwa walegwa wametekeleza agizo la Mkuu wetu wa wilaya kwahiyo
tunatarajia mambo mazuri katika musimu huu wa kilimo hasa kilimo cha zao la
Pamba’alisema Soka
No comments:
Post a Comment