Taarifa zinaeleza kwamba wanafunzi wa darasa la awali yaani chekechea,la kwanza, la pili na hata madarasa mengine baadhi yao hulazimika kuchimba mchanga kwa mikono katika eneo la uwanja wa mpira wa miguu shuleni hapo kisha hujisaidia haja kubwa na baadae huyafunika.
Alipoulizwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji huo Janeth Mayanja amesema kuwa suala hilo la ukosefu analitambua na tayari wameanza kulishughulikia kwa kujenga choo cha dharura kwa wanafunzi hao ikiwa sambamba na ujenzi wa matundu 16 ya vyoo vya kudumu.
Taarifa kutoka katika shule hiyo zinadai kwamba leo wameanza uchimbaji wa matundu hayo ya vyoo.
Hata hivyo wananchi wameshukuru redio mazingira fm pamoja na serikali ya mji wa bunda chini ya mkurugenzi wake Janeth Mayanja kwa hatua alizozichukua katika kunusuru adha hiyo .
No comments:
Post a Comment