Majaliwa ahamasisha uchangiaji damu –Rorya mkoani Mara - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Tuesday, 16 January 2018

Majaliwa ahamasisha uchangiaji damu –Rorya mkoani Mara



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewahamasisha wananchi kujenga mazoea ya kujitolea damu ili kunusuru maisha ya akinamama wazazi na watoto wakiwemo majeruhi wa ajali wakati wa wanapofanyiwa upasuaji.

Waziri Mkuu alikuwa akizungumza wakati wa kukagua kituo cha afya cha Kinesi wilayani Rorya kilichojengwa kwa fedha za moja kwa moja kutoka serikali kuu.

Waziri Mkuu amewataka viongozi wa halmashauri kuhakikisha wanawahamasisha wananchi kujitokeza katika haraambee za uchangiaji damu ili kutatua upungufu katika benki ya damu katika maeneo yote ya kutolea huduma za afya.

Aidha waziri mkuu akawahiidi wananchi kuwa serikali itahakikisha inapandisha hadhi kituo cha afya cha Kinesi kuwa hospitali ya wilaya huku akielezea mikakati wa serikali inayolenga kuongeza magari ya wagonjwa ili kutatua changamoto ya wagonjwa kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya afya.

No comments:

Post a Comment