Hali ya
upatikanaji maji safi na salama katika mtaa wa Migungani kata ya Bunda stoo halmashauri ya mji wa Bunda mkoa wa Mara
hairidhishi kutokana na huduma hiyo kuwa hafifu katika eneo hilo.
Wakizungumza
na mazingira fm kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema hali ya upatikanaji wa maji inazidi kuwa ngumu
kutokana na ukame unaokabili maeneo.
Stivine
Warioba mkazi wa migungani amedai kuwa mamlaka ya maji katika halmashauri ya
mji BAWASA, wamekataa uuzaji wa maji katika mabomba ya watu binafsi kutokana
kutojaza mikataba ya awali ya kuuza maji .
Naye
mwenyekiti wa mtaa wa migungani bwana Elias Robati amekiri kuwepo tatizo la
maji na tayari linafaniwa ufumbuzi ikiwemo kukusanya michango mbalimbali kutoka
kwa wananchi kuweza kusambaza line kubwa ya mabomb.
Aidha
wananchi hao wameiomba halmashauri ya mji huo kutatua tatizo hilo haraka kwani
imekuwa ni kero kwani wanawake na watoto
ndiyo wenye kupata adha hiyo
No comments:
Post a Comment