Imeelezwa
kuwa Mkurungezi wa Mamlaka ya maji Bunda BUWASA bwana Mansur Mandemula
amesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi kufuatia tuhumu zinazomkabili za kuwa
na duka la vifaa vya huduma ya maji jambo ambalo ni kinyume.
Akizungumza
na radio mazingira fm Kwanjia ya simu Mkuu wa Wilaya Ya Bunda Mwl.Lydia
Bupilipili amethibitisha kusimamishwa kwa mkurungezi huyo na kwamba siku ya leo
ndiyo amekabidhi ofisi ili kupisha uchunguzi.
Bipilipili
amesema tayari bodi ya maji Imevunjwa kutokana na kuwepo kwa taarifa za
kumtetea Mkurungezi huyo huku wakishindwa kutimiza wajibu wao kama bodi na
badala yake wamesababisha hadi deni limefika milioni mia nne sabini na saba
paka sasa hivi.
Aidha
Bupilipili amesema kuwa awali aliwaeleza wajumbe wa bodi hiyo kuwa wao wapo
kwajili ya wananchi na sio watu wengine na kwamba bodi ilionekana kutokuwa
wabunifu katika kazi zao kwa wananchi.
Katika hatua
nyingine Bupilipili amesema moja ya agizo la waziri mkuu ni kutuma wataalam
kutoka Makao makuu TAMISEMI ili kuja kuchunguza miradi yote ya maji katika
Wilaya ya Bunda ambapo tayari wataalam hao wameshafika na tayari wameshaanza
kazi kama maagizo yalivyokuwa.
No comments:
Post a Comment