Wito
umetolewa kwa Jamii ya Mkoa wa Mara kutakiwa
kufanya kazi kwa ukaribu na viongozi wa serikali ili kuhakikisha kuwa vitendo
wa ukatili wa kijinsia vinakomeshwa ndani ya mkoa huo.
Wito huo
umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima wakati akizungumza katika
uzinduzi wa saccos ya wanawake wa halmashauri ya mji wa Bunda siku ya leo
katika viwanja vya ofisi ya halmashauri hiyo.
Malima
amesema hivi karibuni ndani ya mkoa wa Mara kumetokea matukio ya ukatili wa kijinsia
hasa kwa watoto wa kike jambo ambalo sio la kuvumilikaa hata mara moja.
Aidha Malima
amewasihi wa wanawake kuendelea na umoja walionao sasa ili wawe mfano hata kwa
mikoa mingine katika kuelekea uchumi wa kati ndani ya nchi yetu.
Katika suala
la uzinduzi wa SACCOS hiyo ofisi ya mkuu wa Mkoa imechangia Laki tano za kitanzania
ili kuwawezesha wanawake hao katika kujikwamua kiuchumi.
Grace Marwa
ambaye ni mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara yeye katika nafasi yake amekabidhi
hati ya kiwanja chenye thamani ya Milioni Nne huku akiahidi kama saccos hiyo
itaendelea vizuri atatoa mshahara wake wa miezi miwili kuwawezesha wanawake hao
kukuza saccos yao.
Naye
Mkurungezi wa mji wa Bunda Janeth mayanja amewahakikishia wanawake hao kuwa
halmashauri ya mji wa bunda itafanya kazi kwa ukaribuni na Saccos hiyo ambayo
ina jumla ya wanachama 450 na kwamba halmashauri imechangia milioni kumi katika
saccos hiyo.
No comments:
Post a Comment