Wananchi wa
kata Bunda stoo katika halmashauri ya mji wa Bunda mkoa wa Mara wameeleza namna
wamenufaika na huduma ya umeme wa REA ikiwa ni pamoja na kijipatia maendeleo ya
kiuchumi kutokana na huduma hiyo.
Hayo
yamesemwana baadhi ya wananchi wa mashine ya maji na migungani wakati
wakizungumza na mazingira hii leo wamesema huduma ya umeme wa REA umewafikia
walengwa kwa gharama nafuu ya elfu ishirini na saba kuvuta umeme huo ambapo
huduma hiyo imeanza mwaka jana .
Wameongeza
kuwa wengi wao katika maeneo hayo wamenufaika na uhuduma hiyo na wanafaaidika
kutokana na huduma hiyo kuwasaidia katika matumizi ya nyumbani ikiwemo mwanga
na kuchaji simu pia wanajipatia uchumi kupitia huduma hiyo ikwa ni pamoja na
miradi inayotegemea umeme huo kama kuchajisha simu kuwaingizia kipato.
Aidha
wamemuomba diwani wa kata ya bunda stoo kutembelea wakazi wa maeneo hayo
kuwasikiliza matatizo yao ikiwemo tatizo la maji ambapo limekuwa tatizo katika
maeneo mbalimbali ya mji wabunda.
No comments:
Post a Comment