Jeshi la Polisi mkoa wa Mara
linawashikilia watu zaidi ya 40, wakazi wa Kijiji cha Mikomariro wilayani
Bunda kwa tuhuma za mauaji ya watu wawili sababu ikitajwa kuwa ni mgogoro wa
mpaka wa shamba.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara,
Jafari Mohamed amethibitisha kukamatwa kwa watu hao huku akiongeza kuwa Jeshi
lake bado linawasaka watu wengine waliohusika na tukio la mauaji ya watu wawili
wakazi wa Kijiji cha Remng'orori wilayani Serengeti.
Aidha kamanda Jafari amebainisha
kuwa waliokamatwa ni wale walioshiriki yowe iliyosababisha mauaji ya watu
wawili kwa kuwakata kwa mapanga kwa sababu ya ugomvi wa mipaka ya mashamba.
Amesema kuwa chanzo cha mgogoro huo
ni mpaka wa wilaya za Bunda, Serengeti na Butiama ambao unahusisha eneo la
ekari 3,535 ambapo Wegesa Gikene na Nyamhanga Gembo wakazi wa Kijiji cha
Remng'orori waliuawa kwa kukatwa na mapanga wakati wakiwa shambani.
No comments:
Post a Comment