BAKAR
Khamis (25) mkaazi wa Mitondooni Wilaya ya Wete, anadaiwa kumnajisi (kumlawiti)
mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka minne huko Shehia ya Piki Wilaya hiyo.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi baba mzazi wa mtoto huyo
alisema mtuhumiwa alimchukuwa mwanawe hadi Bahanasa na kuingia
kwenye gari ya abiri na kumpeleka bonde la Hindi na kumfanyia ulawiti.
Alisema mtuhumiwa
ni mgeni katika shehia hiyo, alikwenda kwa kutembea, ingawa alichokifanya ni
kumchukua mtoto wake na kwenda kufanyia kitendo cha ulawiti, jambo ambalo
linamtia huzuni kila anapofikiria.
“Huyo
mtuhumiwa ni mgeni hapa kijijini kwetu, alipoona tu washamzoea watoto ndipo
alipoamua kumchukua mwanangu kwenda kumlawiti na huko kwao tumesikia kaondoshwa
kwa kuwafanyia watoto kitendo hicho”, alisema baba huyo.
Kwa upande
wake mama wa mtoto, alisema aliondoka na kwenda mazikoni, ambapo
mara baada ya kufika alipigiwa simu na kuambiwa kuwa mwanae amemfuata na ndipo
alipofanya haraka ya kurudi, ingawa alipofika hakumkuta.
“Alimpelea
katika bonde la Tangoni – Hindi na wakati anamlawiti wakatokea watoto
wanaochuma mabungo na mtuhumiwa akakimbia, ndipo walipomuuliza anapoishi na
kusema na wakamleta nyumbani”, alisema mama huyo.
Alieleza
mara baada ya kufika mtoto wao walimuhoji na kusema kuwa kaka Bakar, alimchukua
na kwenda kumfanyia kitendo cha ulawiti na kisha kumpa maandazi, ambapo
aliporudi alikuwa nayo kwenye mfuko.
“Walikuja
wazazi wa upande wa mtuhumiwa tufanye suluhu ili tusiifikishe kesi Polisi,
lakini kwa kitendo alichofanyiwa mwanangu siwezi kusamehe, kwani huu ni
ukatili”, alisema mama huyo.
“Huyu
mtoto ana kawaidi ya kucheza na mwanangu, sasa alikuja mwanangu na kilio na
kuniambia kaka ananikimbia, nikatoka nje nikamwita lakini na mtuhumiwa ikawa
anamwita, sasa ikawa kama tunavutiana, ingawa sikuwa na wasiwasi nae nikaona
labda anamfuata tu kwa vile washamzoea”, alisema jirani wa mtoto huyo.
Nae,
kijana mmoja anaeishi mtaa huo, alisema alimshuhudia mtuhumiwa akiingia kwenye
gari na mtoto huyo maeneo ya Bahanasa na kuteremka Mzambarauni majira ya saa
3:00, ingawa hakujua alikompeleka kutokana na yeye alikuwa anaenda Wete.
“Mimi
sikufanya wasiwasi maana nilijua ni mdogo wake wa maduguni, kwa hiyo niliporudi
ndio nikapata taarifa hiyo na ndipo nilipokumbuka wakati nilipomuona anapanda
nae gari”, alisema kaka huyo.
Mratibu wa
shehia ya Piki, Bikombo Shazil Makame, alisema tukio hilo limetokea katika
shehia yake na tayari wameshalifikisha kituo
cha Polisi Wete, ambapo aliwataka wazazi kuwa mstari wa
mbele kwenda kutoa ushahidi mahakamani, ili kesi iweze kupata hatia.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Haji Khamis Haji, alisema tukio hilo
lilitokea Januari 2 mwaka huu saa 6:00 mchana huko Piki, mtuhumiwa huyo
alimnajisi mtoto wa kiume mwenye miaka minne shehia ya Piki Wilaya ya Wete.
Kamanda
huyo, alisema mtuhumiwa huyo ameshakamatwa na Jeshi hilo linaendelea na
upelelezi, ambapo watampeleka mahakamni mara baada ya uchunguzi kukamilika
kujibu tuhuma zinazomkabili.
No comments:
Post a Comment