Imeelezwa kuwa Halmashauri
ya mji wa Bunda Mkoani Mara kwa mwaka wa fedha 2017/18, ilikisia kupokea na
kutumia jumla ya shilingi bilioni ishirini Milioni mia sita stini, laki tisa na
saba Elfu miambili tisini na saba kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato.
Akifungua Mkutano wa
baraza la madiwani wa halmashauri hiyo Mwenyekiti Pius Mayaya amesema kwamba
mpaka januari mwaka 2018 mtiririko wa fedha kutoka serikali kuu haukuwa mzuri
kwa vyanzo vyote vikuu yaani fedha za matumizi ya kawaida na fedha za miradi.
Ambapo amedai kuwa hadi
kufikia januari mwaka huu fedha walizopokea ni shilingi bilioni nane milioni
miatisa thelathini na tatu laki sita tisini na tano elfu na mia mbili themanini
na tisa na senti sitini na sita ambazo sawa na asilimia 43.4% ya bajeti kisiwa.
Aidha kwa mwaka wa
fedha 2018/19 halmashauri ya mji huo umepitisha bajeti ya zaidi ya shilingi
bilioni 25 zitakazotumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Pia Mayaya amesema kwa
mwaka huo wa fedha wanatarajia kuajiri watumishi 426 katika idara mbalimbali
ikiwa ni sambamba na watumishi 394 wanatarajiwa kupandishwa vyeo.
No comments:
Post a Comment