Halmashauri kuu Chama cha Mapinduzi CCM katika wilaya ya Bunda
mkoani Mara, kimepitisha azimio la kumkataa mkuu wa wilaya hiyo, na kumuomba
Rais Dk. John Magufuli kumhamisha, kwani atasababisisha maendeleo katika wilaya
hiyo kukwama.
Azimio hilo limefikiwa baada ya kikao cha halmashauri kuu ya
chama hicho kukaa jana ikiwa ni sehemu ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa
ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM kuanzia July 2017 hadi December 2017.
Hata hivyo kimekataa kupokea taarifa ya mkuu huyo wa wilaya ya utekelezaji wa ilani ya CCM aliyokuwa
anaiwasilisha ambapo wamedai kuwa ina mapungufu mengi.
Katika hatua nyingine mwenyekiti wa CCM mkoani Mara, Samweli
Kiboye maarufu kwa jina la namba tatu, amesema mkuu wa wilaya ya Bunda, pamoja
na mkuu wa wilaya ya Tarime ni mzigo kwa chama hicho.
No comments:
Post a Comment