Diamond amtia matatani Askari Magereza - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Monday, 12 February 2018

Diamond amtia matatani Askari Magereza

STAA wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, anadaiwa kumtia matatani askari magereza mmoja ambaye jina halikupatikana mara moja, Ijumaa Wikienda lilishuhudia mkanda mzima.

Ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika Kitengo cha Ustawi wa Jamii, askari huyo alisahau kofia yake ya kazi yenye Krauni ya Bibi na Bwana kwenye kiti aina ya ‘benchi’ ambapo Diamond alipofika aliikalia, jambo ambalo ilielezwa kuwa si sawa kwa sheria za kiaskari.

Ijumaa Wikienda lilimshuhudia askari huyo akinyanyuka haraka kwenye benchi hilo kisha kumpisha Diamond na mwanasheria wake ambao walikaa na kuendelea na mazungumzo yao wakati mlinzi wa msanii huyo, Mwarabu Fighter akichukua sendoz za Diamond zilizokuwa zimekatika na kwenda kuzishona.

Wakati Mwarabu akichukua sendoz hizo, Diamond alishuhudiwa akirudi nyuma na kuikalia kofia hiyo yote bila kujua huku askari huyo akihaha kuitafuta kofia hiyo.

Hata hivyo, askari huyo alikuja kuiona na kofia hiyo baada ya Diamond kusimama, jambo ambalo liliwasababisha askari wenzake akiwemo mkuu wao kumuita na kumuonya mwenzao kuwa alikuwa amefanya kosa kubwa la kisheria za kipolisi.

Ijumaa Wikienda lilipotaka kujua kosa alilolifanya askari huyo lilimuuliza mmoja wa maafisa hao ambaye hakutaka kutajwa kwa kuwa siyo msemaji wa jeshi hilo ambapo alisema kuwa, kofia za askari ni sehemu ya sare na ni kosa kubwa kutoka mwilini mwa askari na kuchezewa kwa kujua au kutojua na raia wa kawaida.

“Kimaadili ya kazi ni sawa na bunduki ndiyo maana kijeshi ukiona askari amevuliwa kofia na mkuu wake, ujue huo ndiyo mwisho wa kazi yake. Maana yake anakuwa amepoteza sifa za kulitumikia jeshi.

“Huyo askari amshukuru Mungu kwa kupewa tu onyo, lakini angeweza kupoteza kabisa sifa ya kulitumikia jeshi la magereza,” alisema mmoja wa maafisa wa jeshi la magereza aliyeeonekana kuwa na cheo kikubwa tofauti na wengine.

No comments:

Post a Comment