DRC wafanya Ibada maalum kuwaombea waliouwawa katika maandamano - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Saturday, 10 February 2018

DRC wafanya Ibada maalum kuwaombea waliouwawa katika maandamano

kongo
Image captionIbada maalum kuwaombea waliouwawa katika maandamano ya kumpinga Rais Kabila
Kanisa katoliki nchini DRC imefanya misa maalum ya kuwakumbuka raia saba ambao walifariki katika maandamano yaliyofanyika Januari 21.
Misa hiyo iliitishwa na viongozi wa kanisa katoliki kuwaombea waandamanaji waliouwa kwa risasi wakitaka Rais Kabila kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa Decemba mwaka 2016.
Wafuasi wengi wa upinzani walikutana katika kanisa Katoliki la Notre Dame Du Congo, na Padri Luyeye aliongoza misa hiyo.
DRC
Image captionIbada ya kuwakumbuka waliouwawa DRC
Padri huyo alinukuliwa akisema "wakristu wataendelea na vita hadi tutapata mama na baba ambae anastahili kuongoza nchini na pia atakaye heshimu haki ya raia"
Wafuasi wa upinzani walifurika kwa wingi katika misa hiyo huku wakisema wataendelea kuunga mkono mpango wa kanisa katoliki wa kufanya maandaano
Watu zaidi ya kumi wameripotiwa kuuwawa toka decemba 31 mwak 2016 kutoka na kumpinga rais wa sasa wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo kuendelea kuwepo madarakani.

No comments:

Post a Comment