Imeelezwa
kuwa Halmashauri ya mji wa Bunda Mkoani Mara imeshakamilisha utaratibu wote wa maelekezo
yaliyotolewa na serikali kuhusu kuwapeleka
wale walimu wa ziada kutoka shule za
sekondari kwenda shule za msingi.
Akizungumza
na Mazingira Fm mwishoni Afisa elimu sekondari wa Halmashauri ya mji wa Bunda Mtundi
Nyamhanga ofisini kwake amesema Walimu 43 ndio waziada ndani ya Halmashauri na
kwamba wote 43 wameshapangiwa vituo vya kazi kama ilivyoelekezwa.
Nyamhanga
amesema wapo baadhi ya walimu kipindi maelekezo yanatoka waliomba wenyewe
wapelekwe msingi na wapo wengine baadhi waliomba wasipelekwe msingi huku
wakitoa sababu za kwanini wasipelekwe huko.
Pamoja na
hayo Mtundi amesema wao kama ofisi walizingatie maelekezo ya serikali kama
ilivyoelekezwa na sio vinginevyo.
No comments:
Post a Comment