Mbunge wa Tarime Vijijini, John
Heche amedai litakuwa jambo la ajabu kwa Watanzania kunyamazia ubaguzi wa vyama
unaofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ikiwa walikuwa mstari
wa mbele kupinga ubaguzi wa rangi.
Heche ametoa kauli hiyo ikiwa ni
muda mfupi baada ya habari za Mkuu huyo wa Mkoa kusambaa akiweka wazi wilayani
Mbulu kwamba hayuko tayari kutoa msaada kwa diwani wa chama cha upinzani
kwa kuwa yeye anatekeleza ilani ya chama kilichopo madarakani.
Heche amesema kutokana na kauli hiyo
iliyotolewa na kiongozi huyo mkubwa wa mkoa anasubiri kusikia kauli ya Chama
chake na rais aliyemteua Mnyeti.
Aidha Mbunge huyo amesisitiza kwa
kusema kwamba Ubaguzi ni ubaguzi tu uwe wa rangi, kabila,dini au hata vyama.
No comments:
Post a Comment