MWANAMUZIKI ambaye hivi karibuni
aliachia wimbo wake uitwao Mipaka, John Simon ‘Joh Makini,’ amefungukia
kupotezwa kimuziki na baadhi ya wanamuziki wanaofanya vizuri kwamba si kweli,
bali wanaosema hivyo hawafuatilia vizuri muziki wake.
Akichonga na Full Shangwe, Joh
alisema kwamba kabla ya watu kuzungumzia juu ya kupoa kwake kimuziki, tofauti
na kipindi cha nyuma inabidi waangalie kazi anazofanya na nini kilimfanya
asikike sana kuliko wakati huu.
“Si kweli kwamba nimepoa kama
ambavyo watu wanakuwa wanazungumza huko kwenye mitandao, mimi bado nipo vizuri
na kazi zangu zinafanya poa, zaidi sitegemei kuchuja hata siku moja,” alisema
Joh.
No comments:
Post a Comment