Wakazi wa
mtaa wa Kilimahewa kata ya Kabalimu Halmashauri ya mji wa Bunda wameiomba
serikali kujenga tenki la maji katika vilima vya Kilimahewa ili kutatua tatizo
la maji katika mtaa huo wenye wakazi 2000.
Ombi hilo
limetolewa na mdau wa maji bwana MUSA
MADUKA alipokuwa akizungumza na radio mazingira fm leo kutokana na uhaba
mkubwa wa maji unaowakumba wananchi hao.
MUSA MADUKA amesema kuwa kutokana na taarifa
yake aliyoiwasilisha idara ya maji ya mji wa bunda ameiomba serikali kuifanyia
kazi ili kuwapunguzia wanawake wa mtaa huo kutembea umbali mrefu ili kutafuta maji.
Mkazi wa
mtaa huo SIMON BALOLAGE amesema kuwa
ni vizuri serikali ikaharakisha kujenga tanki hilo ili kuwarahisishia wananchi
hao upatikanaji wa maji safi na salama.
Kwa upande
wake mdau wa maji mji wa Bunda SULEIMAN
NASSORO ameeleza kuwa kuna mpango wa kujenga tenki la maji katika vilima
vya kilimahewa ili kuongeza nguvu ya maji ili kutatua kero ya maji.
No comments:
Post a Comment