Kiongozi wa taifa la Korea Kaskazini Kim Jong un amemualika rais wa Korea Kusini Moon Jae-in kuzuru Pyongyang.
Utakuwa mkutano wa kwanzakatika kipindi cha zaii ya mungo mmoja katika ya viongozi hao wa Korea.
Bwana Moon amesema kuwa Korea ni muhimu kuhakikisha kuwa mkutano huo unafanyika huku akiitaka Korea Ksakzini kurudi katika meza ya mazungumzo na Marekani.
Mualiko huo ulioandikwa ulikabidhiwa kwa rais wa Korea Kusini na dadake rais Kim Jong un , Kim Yo Jong.
- Idadi ya wanaohama Korea Kaskazini wakienda Korea Kusini yapungua
- Korea Kaskazini yakataa mazungumzo na Korea Kusini
- Dadake rais wa Korea Kaskazini awasili nchini Korea Kusini
Katika mkutano wa kihistoria uliofanyika katika jumba la rais kabla ya kuanza kwa michezo hiyo ya msimu wa baridi.
Bi Kim na kiongozi wa kisherehe wa taifa la Korea Kaskazini Kim Yong-nam ndio viongozi wa ngazi za juu kutoka Kaskazini kuzuru kusini tangu vita vya Korea 1950.
Viongozi hao kutoka Korea hizi mbili walikula kabeji, wali na kuzungumza kwa takriban saa tatu.
Wakati huohuo Rais wa Korea ya Kusini Moon Jae amekuwa ni mwenye shughuli nyingi za kupokea ujumbe wa ngazi ya juu katika ikulu yake ya mjini Seoul, baada ya ufunguzi rasmi jana wa michezo ya Olympic ya msimu wa baridi nchini humo.
Ujumbe unaoangziwa zaidi ni ule wa Korea ya kazkazini ambapo jana ameamkuana na dada yake kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong un
Ulikuwa ni mara ya kwanza ujumbe kama huo wa maafisa wa ngazi za juu zaidi wa Korea Kaskazini kuwahi kuzuru Korea Kusini tangu kumalizika kwa vita vya Korea miaka 60 iliyopita.
Hata hivyo hatua hiyo haijafurahiwa na Marekani.
Makamu rais wa Marekani, Mike Pence alisusia mwaliko wa chakula cha jioni ambacho alitakiwa kukaa meza moja na kiongozi wa serikali ya Korea Kaskazini Kim Yong-nam.
Taarifa kutoka chombo cha habari cha Yo hap kimesema kuwa Pence alionana kidogo na bwana Kim wakati wakijaribu kukwepana kuonana uso kwa uso.
Michezo hiyo inaendelea wakati ambapo kuna mvutano juu ya mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini ambao unapingwa vikali na majirani zake na vilevile Marekani.
Katika shughuli hiyo, Bwana Moon alisema anatarajia mashindano hayo ya michezo ya Olimpiki msimu wa baridi yataweza kukumbukwa kama siku nzuri ya kuanza kuwa na amani.
No comments:
Post a Comment