Kituo cha Radio mazingira fm kimepongezwa kwa kuibua na
kuripoti matatizo mbalimbali ndani ya jamii.
Pongezi hizo zimetolewa na Afisa ustawi wa jamii halmashauri
ya mji wa Bunda Pius Masalu kupitia kipindi cha Duru za habari jioni leo huku Akitolea
mfano wa tukio la mama mmoja aliyetelekeza watoto wawili mmoja akiwa ni mtoto
wake na mwingine akiwa ni mjukuu wake katika mtaa wa Majengo kata ya nyasura
ambapo amesema amepata taarifa ya tukio hilo kupitia radio Mazingira fm.
Sambamba na hilo pia amesema kuwa kazi inayofanywa na radio
mazingira ni jambo la kujivunia katika Halmashauri ya mji wa Bunda na hata Mkoa
wa mara na maeneo jirani inakofika ambapo 91.7 Mazingira akisema kuwa imekuwa ni
msaada mkubwa kwa jamii kutokana wanafanyakazi wake kutokuchoka kufika ndani ya
jamii na kuibua na kuripoti matatizo mbalmbali.
Hata hivyo ametoa wito kwa uongozi na timu mzima ya kituo cha
radio kuendelea na kasi hiyo ili jamii iendelee kunufaika na uwepo wao ndani ya
jamii.
No comments:
Post a Comment