Makamu wa rais awahakikishia wananchi upatikanaji wa dawa za kuuwa wadudu waharibifu wa pamba-Busega Simiyu - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Monday, 19 February 2018

Makamu wa rais awahakikishia wananchi upatikanaji wa dawa za kuuwa wadudu waharibifu wa pamba-Busega Simiyu



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Simiyu kuwa Serikali itamaliza kabisa tatizo la uhaba wa dawa za kuuwa wadudu waharibifu wa zao la pamba.

Mhe. Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Busega kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Lamadi wakati akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake Mkoani Simiyu.

Amesema awamu ya kwanza ya dawa zimeshafika Simiyu kwa ajili ya kuwagawia wakulima wa pamba na akaahidi kuwa awamu ya pili ya kuleta dawa hizo inamalizika katika wiki inayoanza leo tarehe 19/02/2018, hivyo tatizo hilo litakuwa limekwisha.

Katika hatua nyingine Mhe.Makamu wa Rais wakati akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Masanzakona baada kuweka  jiwe la msingi mradi wa maji wa Kiloleli amewahimiza wananchi kuchangia huduma za maji ili miradi ya maji iwe endelevu.

No comments:

Post a Comment