Makubwa haya !! mwanaume agoma kujisaidia haja kubwa kwa zaidi ya siku 20 - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Saturday, 10 February 2018

Makubwa haya !! mwanaume agoma kujisaidia haja kubwa kwa zaidi ya siku 20

Mwanaume mmoja nchini Uingereza amekuwa agenda katika mijadala siku za hivi karibuni baada ya kukataa kabisa kujisaidia haja kubwa na hadi sasa zikiwa zimepita siku 20, akihisiwa kuwa anatembea na dawa za kulevya tumboni.

Polisi wanaomshikilia wameeleza kuwa wamekuwa wakimwangalia saa zote kusubiri wakati atakaojisaidia lakini bado hajafanya hivyo, lakini hata hivyo wameeleza kujipanga kwao kuendelea kumweka chini ya uangalizi wao na kusubiri hadi atakapoamua kujisaidia.

Kwenye kutafuta taarifa za kidaktari kuhusu uwezekano wa mtu huyo kuhatarisha maisha yake au la kwa kitendo hicho, Shirika la Utangazaji la BBC Uingereza limezungumza na Trish Macnair, wa Primary Care Society for Gastroenterology.

Trish ameeleza kuwa mwanaume huyo hatoweza kuendelea kukaa bila kujisaidia kwa muda mrefu kama anavyofikiri kwa itafika kipindi mwili utakataa kuendelea kutunza uchafu.


“Utafika muda atasikia tumbo lake likisogea, japokuwa anakataa kula jambo linalofanya urahisi wa kuweza kukaa bila kwenda chooni, tumbo litaanza kusogea tu, kwani litakuwa limejaa chakula ambacho ni uchafu.” – Trish Macnair

No comments:

Post a Comment