Kikosi cha
Simba kitashambulia mfululizo na kwa kasi kubwa katika mechi yao dhidi ya
Gendamarie kutoka Djibouti.
Taarifa
kutoka ndani ya Simba zinaeleza, Kocha Mkuu, Pierre Lechantre amewataka
wachezaji wake kucheza kwa kasi na kushambulia mfulilizo ili kupata mabao ya
haraka.
Mechi hiyo
ya Kombe la Shirikisho Afrika, inapigwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam.
“Kocha
anataka kushambulia na kupata mabao, amewaeleza wachezaji mengi lakini kikubwa
ni umakini katika umaliziaji,” kilieleza chanzo.
Kocha huyo
alikaa na wachezaji wake na kutumia zaidi ya nusu saa akiwaeleza kinachotakiwa
kufanyika katika mechi hiyo ya Gendamarie ambao wanaonekana ni dhaifu.
Hata
hivyo, kocha huyo inaelezwa amewasisitiza kutotanguliza dharau na kuhakikisha
wanashinda kwa mabao idadi nzuri.
No comments:
Post a Comment