Siku chache baada ya
redio mazingira fm, kuripoti habari inayoeza kuwa mwalimu mkuu katika shule ya
sekondari Nansimo kuhusishwa na ubadhirifu wa fedha zilizochangwa na wananchi
hatimae mwalimu huyo ameshushwa wadhifa wake na kuwa mwalimu wa kawaida.
Akizungumza na kituo
hiki leo mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Costantini Mizani amethibitisha kutokea hilo na kueleza kuwa
hatua hiyo imekujia baada ujio wa kaimu afisa elimu wilaya pamoja na afisa
elimu taaluma kufika shuleni hapo kufutilia suala hilo.
Amesema mwalimu huyo
meshushwa cheo kupisha uchunguzi na kwamba tayari amesharipoti mwalimu mwengine
kuchukuwa nafasi yake.
No comments:
Post a Comment