Nay wa Mitego afunguka kuhusu kauli yake kwa Diamond - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Tuesday, 20 February 2018

Nay wa Mitego afunguka kuhusu kauli yake kwa Diamond



Msanii wa muziki Bongo, Nay wa Mitego amefunguka kuhusu kumtabiria Diamond kushuka kimuziki.

Siku za karibuni Nay wa Mitego alipost picha katika mtandao wa Instagram ikionyesha myama simba akiuawa kikatili, picha hiyo iliamsha hasira kwa mashabiki wa Diamond kwa sababu msanii huyo hutumia jina la simba pia.

Nay akizungumza na kipindi cha The Playlist cha Times Fm amesema hakukusudia jambo lolote baya kwa Diamond kwa sababu ni rafiki yake na wameshawahi kufanya kazi pamoja.

“Diamond ni mshikaji wangu, tumefanya kazi kubwa sidhani kama imefikia hatua ya sisi kuwa maadui kiasi hicho na siwezi kumuombea mabaya kiasi hicho lakini tunaona changamoto anazopitia,” amesema Nay.

“Nilijua tu ile picha wabongo kila mtu ataongea la kwake lakini sina tatizo na Diamond na hata kama lipo basi tutalimaliza ile picha ilikuwa haimuhusu,” amesisitiza.

Nay amesema sababu ya kuposti picha hiyo ni kupima akili za mashabiki wala kulikuwa hakuna lolote baya. Nay wa Mitego na Diamond wameshafanya kolabo mbili ambazo ni Muziki Gani na Mapenzi Pesa.

No comments:

Post a Comment