Waziri mkuu akiwa mashine ya maji
Bunda
Mkuu wa wilaya Bunda Mwl.Lydia Bupilipili
Toka amalize ziara yake Waziri Mkuu KASIMU
MAJALIWA mwezi January mwaka huu katika mkoa wa Mara, siku ya
majumuisho ya ziara yake Waziri mkuu alitoa maagizo mbalimbali ikiwa ni
pamoja na agizo la Meneja wa maji Bunda bwana MANSOUR MANDEMLA kukabidhi
ofisi na kupisha uchunguzi kuhusiana na tuhuma mbalimbali zinazoikabili idara
hiyo.
Lakini katika hali ambayo ni ya
kushangaza kidogo siku ya Jana Februari 26 2018 ndio siku ambayo Meneja huyo
amekabidhi rasmi ofisini akiwa chini ya ulizi.
Mapema jana Radio Mazingira ilipata
taarifa kuwa Meneja huyo anakabidhi ofisi baada ya kumalizika mwezi sasa toka
waziri mkuu atoe agizo hilo.
Baada ya taarifa hizo ikabidi kufika
ofisi ya mkuu wa wilaya ya Bunda ili tuweze kufahamu zaidi kuhusiana na suala
hilo maana awali ilisikika kuwa kuna agizo kutoka ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mara
ikimtaka akabidhi ofisini lakini ikwa kimya tena.
Tulipomuliza Mkuu wa wilaya ya Bunda
mwl.LYDIA BUPILIPILI amesema ni kweli Mansour Mandemla amekabidhi ofisi
ili apishe uchuguzi na kwamba wameamua kumsimamia kwa ulizi kutokana kuonekana
akiwazungusha katika kukabidhiana suala ambalo limewakela kama watendaji wa
serikali.
Akiwa katika uwanja wa Sabasaba
mjini Bunda KASIMU alisema kuwa serikali haina nafasi ya
kuwavumilia wale wote wanaoharibu miradi ambayo serikali imetoa pesa ili
kuwasaidia wananchi wake hivyo kabla wananchi hawajapata madhara mtu huyo au
watu hao wataondolewa mara moja kwani inaonekana wazi wameshindwa kutimiza
wajibu wao kikamilifu katika kuwatumikia wananchi
No comments:
Post a Comment