Watanzania Katika
Wilaya Bunda Mkoani Mara wametakiwa kuacha siasa makanisani bali waendelea
kuliombea taifa pamoja na viongozi wake bila kukoma ili amani na utulivu uendelee
kuwepo siku zote katika taifa la Tanzania.
Rai hiyo
imetolewa na Mtumishi wa Mungu Mchungaji Frederick Jumanne katika ibada
takatifu siku ya jumapili katika kanisa la E.A.G.T Chiringe Mjini Bunda ambapo alisema siku hizi
siasa imeingia hadi kanisani katika hali ambayo hata waamini wanashindwa
kuelewa kinachoendelea makanisani.
Jumanne
amesema ni bora watanzania hasa waliowatumishi wa Mungu wakatumia muda wao gi
kuliombea taifa na sio kujiingiza katika mambo ya siasa kwani kufanya hivyo ni
kusahau majukumu uliyopewa kama mtumishi.
Jumanne
amesema maombi ni silaha kubwa katika kumshinda adua yako hivyo watanaznia
wajikite katika maombi ili adui wa Taifa la Tanzania akapata kushindwa.
No comments:
Post a Comment