Sanchez anajilipa mshahara Old Trafford - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Saturday, 10 February 2018

Sanchez anajilipa mshahara Old Trafford


Unaweza kusema mchezaji wa Manchester United Alexis Sanchez anajilipa mwenye mshahara pale Old Trafford kutokana na mkwanja ambao anaiingizia klabu hiyo kupitia vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mauzo ya jezi inayovaliwa na nyota huyo aliyepita vilabu vya Udinese, Barcelona na Arsenal.
Sanchez ndiye mchezaji anayevuta mkwanja mrefu zaidi kwenye ligi ya England akiwa anakunja £350,000 kwa wiki akimzidi Paul Pogba kwa  £60,000 ambaye awali alikuwa analipwa vizuri zaidi kabla ya ujio wa Sanchez.
Mtendaji mkuu wa Manchester United Ed Woodward amesema utambulisho wa mchezaji Alexis Sanchez umevunja rekodi ya mauzo ya jezi kwa timu hiyo pamoja na kupata wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii.
Wakati Manchester United wakikubali kumlipa Sanchez pesa nyingi tayari walishafanya hesabu zao na kujua fedha hizo zitatokana na mapato atakayoiingizia klabu yeye mwenyewe.
Ukiangalia siku ambayo Sanchez  alitambulishwa, utambulisho wake uli-trend sana kwenye mitandao ya kijamii. Account ya instagram ya Manchester United post ya Sanchez ilipata likes zaidi ya milioni mbili kwenye ukurasa wa facebook post ilivunja rekodi ya kuwa-shared mara nyingi zaidi vivyo hivyo kwenye ukurasa wa twitter ilikuwa retwetted mara nyingi zaidi ya post yoyote kuwahi kutokea kwenye account ya twitter.
Maana yake reach ilikuwa ni kubwa, impressions zilikuwa ni nyingi, kadiri inavuosambaa duniani kote hilo ndio lilikuwa lengo lao na silaha yao ya kwanza kuhakikisha watu wengi wanafahamu juu ya usajili wa Sanchez na unakuwa gumzo halafu wanakuja kabla ya kuleta mzigo.
Wakati mwingine ule mvutano kuhusu issue ya usajili inakuwa ni mbinu ya kutengeneza ushawishi na tension kwa watu huko nje. Hata wakati wa photo shoot kwa ajili ya picha na video walikuwa wanaficha ili wakishamaliza na kutengeneza ushawishi kwa watu kutaka kumjua zaidi Sanchez ndio wanachukua mzigo wa jezi wanaingiza sokoni.
Mauzo ya jezi ya Sanchez yamevunja rekodi ya Neymar mara tatu sasa kwa nini wasimlipe pesa nyingi na wasipambane kumchukua? Karibu robo tatu ya wananchi wa Chile walinunua jezi ya Sanchez.
Sababu ya Manchester United kuuza sana jezi ya Sanchez ni wao wenyewe walitengeneza mchakato wa kufanya biashara.

No comments:

Post a Comment