Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Kaunya Yohana Rugembe amefunguka na kudai kuwa kinachokwamisha juudi za Mbunge wa jimbo hilo katika kutatua kero ya Maji ni urasimu unaofanywa na baadhi ya watu walioko madarakani.
Katibu huyo ameyasema hayo wakati akihojiwa katika kituo cha redio mazingira fm kupitia kipindi cha asubuhi leo, ambapo amesema kuwa tatizo la maji mjini hapo lilitengewa fedha za kutosha lakini ubadhirifu ulifanywa na baadhi ya watu wachache.
Amedai kuwa hata wakati Waziri Mkuu wa Tanzania Majaliwa Kasim Majaliwa alipofanya Ziara yake mjini hapo alitoa maagizo ya kumtaka Meneja wa Mamlaka ya maji mjini hapo apishe ofisi kwa uchunguzi lakini kilichotokea meneja huyo aliendelea kuwepo ofisini na hatua hazichukuliwi dhidi take.
Katika hatua nyingine katibu huyo ameeleza kwamba mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini ni mchapakazi lakini anakeamishwa na baadhi ya watu kwa kuangalia itikadi za kisiasa.
Kuhusu kuja jimboni kwake Mbunge Huyo, Kaunya alisema kwamba Ester Bulaya anatarajiwa kufanya ziara jimboni kwake kuanzia siku ya jumatatu wiki ijayo kukagua miradi ikiwa ni pamoja na kupokea kero za wananchi kabla ya kwenda kuyawasilisha Bungeni mwezi wa nne.
No comments:
Post a Comment