Video: Kibao kingine cha Mbosso chini ya WCB ”Nimekuzoea” - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Saturday, 10 February 2018

Video: Kibao kingine cha Mbosso chini ya WCB ”Nimekuzoea”


Msanii wa nyimbo za bongo fleva ambaye hivi karibuni amesajiliwa katika kundi la WCB, Marombosso baada ya kimya cha muda mrefu kutanda kutokana na kundi alilokuwa akifanyia kazi, Yamotoband kusambaratika, Marombosso sasa ameanza kuachia nyimbo zake ambazo zinafanya vizuri.
Ni siku chache tu tangu Marombosso asajiliwe katika kundi la WCB, kazi zake zinaanza kuonekana na uamuzi wake wa kujiunga na kundi hilo unazaa matunda yanayonekana.
Ndani ya wiki mbili Marombosso ameweza kuachia nyimbo zake mbili na sasa anatamba na kibao kinachoitwa ”Nimekuzoea”, ambacho hadi sasa umekwishatazamwa na watu 158,463 ikiwa ni siku moja tu tangu kuachiwa kwa ngoma hiyo.
Bonyeza link hapa chini kuitazama video hiyo na kuendelea kusapoti muziki wa Mbosso na muziki wa ndani, Bongo fleva.



No comments:

Post a Comment