Waandishi wa Habari
kutoka Redio za Kijamii Tanzania
wametakiwa kutumia fursa zinazotolewa na Shirika la Umoja Wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni –UNESCO-ili kuleta mabadiliko kwa Jamii.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti
wa Mtandao wa Redio za Jamii Tanzania –TADIO -,PROSPER KWIGIZE katika mafunzo yanayoendelea mjini
DODOMA,yanayo shirikisha waandishi wahabari 49 kutoka redio 24 zajamii.
Bwana KWIGIZE
amesema mafunzo kwa waandishi wahabari hususani katika maeneo yamazingira na jinsia
hutolewa kwakulipia kiasi cha ada lakini UNESCO hutoa mafunzo kama hayo bila malipo
yoyote.
Amesema ni vyema kuthamini
na kuzingatia elimu wanayoipata waandishi katika mtandao wa TADIO na kuifanyia kazi
kwa manufaa ya jamii.
Kwa upande wake
Mkufunzi wa Mafunzo hayo ROSE HAJI MWALIMU ametoa wito kwa waandishi wa habari kutoka
redio za kijamii kuibua changamoto zinazochangia kuleta usawa katika masuala ya
kijinsia.
No comments:
Post a Comment