vifurushi vya midoli ya ngono
Muungano wa wanafunzi wa chuo kikuu nchini Canada wamepatwa na mshangao pale walipopokea mzigo wa kushangaza wa vifurushi vya midoli ya ngono mpaka taa.
Mizigo isiyotarajiwa iliyotumwa kupitia kampuni ya Amazon kwa watu zaidi ya kumi katika jumuiya hiyo ya wanafunzi.
Kuna ambao wamepokea mizigo mingi kama vifurushi 15 tangu mwezi Novemba,inayogharimu kiasi cha dola 1,000 kwa jumla.
Wengi walidhani kuwa ni mapambo yenye gharama kubwa lakini polisi wameanza uchunguzi juu ya suala hilo.
Inasemekana kuwa mizigo hiyo inaweza kuwa ni njama za kibiashara kutoka nchini China.
Mizigo hiyo iliyojumuisha chaja za simu,taa,simu aina ya ipad pamoja na midoli kadhaa ya ngono.
Amazon wamesema kuwa hawawezi kuzichukua bidhaa hizo ,kwa kuwa zililetwa katika daraja la tatu .Aidha Kampuni hiyo imesema itafanya uchunguzi lakini imewaambia wanafunzi kuwa haiwezi kutaja taarifa za mtu aliyefanya manunuzi kwa sababu ni za siri.
Rais wa muungano wa wanafunzi ametaja kuwa kupokea mzigo huo ni jambo linalostaajabisha sana.
Na kudai kuwa kwanza alidhani labda mzigo huo ni kwa ajili ya mfanyakazi wa chuo ndio ameagiza na anaona aibu kuudai,lakini alipobaini kuwa mzigo umeandikwa kwa ajili ya jumuiya ya wanafunzi nchini Canada, wakasema sawa,baada ya kusikia kuwa kuna idadi kubwa ya wanafunzi wamepokea hivyo wakaona kuwa na kuna jambo linaloendelea.
Chanzo-BBC
No comments:
Post a Comment