Waandishi wa
habari wa redio za Kijamii nchini Tanzania wametakiwa kuzingatia maadili ya
taaluma zao kwakuandika habari zenye tija kwa jamii .
Wito huo
umetolewana Mkufunzi wa Taaluma ya habari kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la
Elimu, Sayansi na Utamaduni-UNESCO-Bi. ROSE HAJI MWALIMU kwenye mafunzo ya siku
nane yanayoendelea Mjini Dodoma.
Amesema ili
jamii inufaike na uwepo wa redio hizo, ni vyema waandishi wa habari kuzingatia miiko na misingi
inayowaongoza kwa manufaa ya umma.
Kwa upande
wao waandishi wa habari wa radio za kijamii wamelishukuru shirika la UNESCO kwa
kuwapatia mafunzo hayo ambayo yatawasidia
kuboresha utendaji kazi katika vituo vyao.
Haya ni
miongoni mwa mafunzo yanayoendeshwa na Shirika la UNESCO kuzipa uwezo redio za
kijamii ili kuandaa habari na vipindi bora.
No comments:
Post a Comment