Wanahabari watakiwa kuzingatia maadili - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Sunday, 11 February 2018

Wanahabari watakiwa kuzingatia maadili



Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuzingatia maadili ya taaluma yao wanapotekeleza majukumu ili kuepusha migogoro katika jamii.
Wito huo umetolewa mjini Dodoma na Mwezeshaji ROSE MWALIMU katika Mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa Habari vijijini  kuandaa vipindi bora yanayoendeshwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni-UNESCO-.
Amesemakutozingatia maadili kama vile ukweli na vyanzo sahihi kutasababisha vyombo vyao kutoaminika na Jamii husika.
Waandishi wa habari 49kutoka Redio za jamii 24 nchiniwanashiriki mafunzo hayo ya siku saba ambayo yameanza Februari 06, hadi Februari 12 Mwaka huu.

No comments:

Post a Comment