SERIKALI mkoani Mara imewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa watafiti wakati wa utafiti wa Mapato na na matumizi ya kaya binafsi Tanzania bara wa mwaka 2017/2018 unaoendelea nchini hivi sasa.
Mkuu wa mkoa Mara, Adam Malima alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambap[o alisema utafiti umeanza na unaendelea ndani ya mkoa wa Mara.
Alisema Utafiti huo wa mapato na matumizi ya kaya binafsi Tanzania bara unatarajia kukusanya taarifa kutoka katika kaya binafsi katika Nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja wanakaya, uzazi na unyonyeshaji.
“Lakini pia utafiti huu wa kaya binafsi utahusisha elimu, afya, uraia, uhamiaji, ulemavu, Bima, hali ya ajira, biashara na mapato ya kaya na makazi ya kaya” alisema Malimu.
Taarifa zingine zitakazokusanywa ni matumizi na nishati, huduma za maji safi, na maji taka, utalii wa ndani, uwekezaji wa kaya, matumizi ya huduma za kifedha , upatikanaji wa usalama wa chakula, matumizi, mazingira na umiliki wa vitambulisho mbalimbali.
Utafiti utajumuisha pia kilimo na mifugo, matumizi ya muda kwa kila mwanakay mwenye umri wa miaka 5 kuendelea, mapato na matumizi ya kila kaya na mawanakaya.
Malima alifafanua kuwa Ofisi ya taifa ya Takwimu ni taasisi inayofanya kazi zake kwa mujibu wa sheria mpya ya takwimu ya mwaka 2015 ambapo wa mujibu wa sheria kifungu cha 37(3)kinataka ushiriki wa wananchi katika utafiti mbalimbali zinazokusanywa na serikali.
Alisema kwa mujibu wa sheria ya takwimu namba 9 ya mwaka 2015 taarifa zinazokusanywa kutoka kila kaya pamoja na wanakaya zitatunzwa kwa usiri mkubwa kama inavyotakiwa.
Aidha mkuu wa mkoa huyo alitaja baadhi ya maeneo yatakayohusishwa na utafiti kama sampuli mkoani humo ni kiongera, Nyarero,Kenyamosabi, Magoma, Nyangoto, Kitenga na Nyabitocho katika wilaya ya Tarime.
Wilaya ya Serengeti ni Kijiji cha Nyiboko,Natta mbiso, Nyanungu, Mbirikili, na Bomani ambapo wilaya ya Musoma vijijini ni Bugunda, Muhoji, Bwai Kumsoma na Kigeraetuma.
Alitaja Vijiji katika wilaya ya Bunda kuwa utafiti utahusisha Manchimweru, Serengeti, Kigaga, Karukekere, Nyamakokoto na Balili, wakati katika Manispaa ya Musoma ni Nyasho Magereza, Mlimani, Mkinyerero, wilaya ya Rorya ni kijiji cha Rwang’enyi, Kyariko, Sakawa, Nyanduga na Kwibuse.
Katika Wilaya ya Butiama utafiti utakuwa katika vijiji vya Masurura, Mirwa, Kyatungwe na Busirime na kwamba kwa kila kaya watahojiwa kwa muda wa siku 14..
No comments:
Post a Comment