Wameeleza kuwa mtendaji huyo ameendesha msako huo kwa madai ya kuwa wananchi ho wameshindwa kushiriki maendeleo ya ujenzi wa shule ya msingi unaoendelea kijijini hapo .
Mashaka Charles mkazai wa kitongoji hicho amesema kuwa hakuwa nyumba ni na wakati amerudi amekuta mtendaji huyo amechukua sola yake kwa madai ya kutohudhuria maendeleo licha ya kutokuwa na taarifa ya uwepo wa kushiriki maendeleo hayo kwa siku hiyo.
Ameongeza kuwa pamoja na kufanyiwa kitendo hicho lakini mtendaji huyo amekuwa mungu mtu kwani amekuwa akitisha kuwafunga watu pindi anaposhauriwa.
Naye Gaudensia Philipo mkazi wa kitongoji hicho amesema mtendaji alipofika kwake amevunja mlango na kuchukua mbuzi,baada ya kumuuliza kwanini anafanya hivyo mtendaji akamweleza kwanini hawaendi kwenye maendeleo.
Amesema licha ya kupokonywa mbuzi wake kwa kutoshiriki maendeleo awali aliruhusiwa kutokwenda maendeleo kutokana na ujauzito alionao.
Majura Apolinary pamoja na Majige Gerad ambao pia ni wananchi
wa kitongoji cha Nyamigunga waliochukuliwa 'solar' suala hilo hawajapendezwa nalo
na wanafanyiwa unyanyasaji hivyo wanaiomba serikali iwasaidie.
Aidha mwenyekiti wa
kitongoji hicho Bwana KASALU KISHOSHA ameeleza kwamba jambo hilo limetokea
katika kitongoji chake na kwa familia zinazokadiriwa kufikia 70 licha ya
wachache tu ndio walioamua kwenda polisi.
Amesema kama mwenyekiti
wa eneo husika alimshauri mtendaji huyo kutotumia utaratibu huo wa kuchukua
maamuzi ya kuvunja milango na kuchukua mali za wananchi wakiwa hawapo katika
kaya zao.
Modestusa Chama ni
mtendaji wa kata ya Nyamag’uta jirani na kata ya Sazira amefafanua suala hilo
kama ukiukwaji wa utaratibu kwani kwa mujibu wa sheria mtu anaegoma kushiriki
maendeleo anatakiwa kuandikiwa samas ya
kuitwa mahakamani ili akahojiwe ni kwanini asichukuliwe hatua kwa kukwamisha
maendeleo.
Hata hivyo kwa upande
wa Mtendaji wa kijiji hicho bwana Jonson
Charles amekiri kufanyika kwa msako huo, ambapo ameeleza kuwa wamezingatia
utaratibu uliowekwa na wananchi wenyewe katika mkutano wa wananchi kupitia sheria
ndogo walizojiwekea ya kukamata mali pindi mtu anaposhindwa kushiriki maendeleo
bila taarifa.
Amesema jumla ya kaya
35 zilifikiwa na msako huo ambapo,baada ya hutua hiyo wananchi walienda polisi
lakini wakashauriwa waende wakae pamoja na uongozi kamaliza tatizo hilo.
Ameongeza kuwa
makubaliano walioweka ni mwananchi kukomboa mali zake kwa kutoa shilingi elfu
tano na mpaka sasa tayari wameshajitokeza waliofanya hivy na jumla ya shilingi
laki moja imepatikana-100,000/-.
Naye Diwani wa kata ya
Sazira Bwana Jumanne Mnyaruga amedai kuwa wananchi hao kukimbilia vyombo vya
habari na polisi siyo suluhisho badala yake wanapaswa kukaa na uongozi wao ili kupata
muafaka.
No comments:
Post a Comment